Kamati ya PIC Yaitaka Serikali Kuisaidia TTCL Ijiendeshe Kibiashara
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka Serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuiwezesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujiendesha kibiashara...