TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI WA TAARIFA ZA MIFUMO YA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA TTCL KUVAMIWA NA WADUKUZI.



Nicodemus Mushi,
Meneja Uhusiano TTCL

Jumanne, Februari 16, 2016, Katika Website ya Soft Pedia kulichapishwa taarifa kuwa Mifumo ya Mawasiliano ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL imevamiwa na Wadukuzi na kwamba taarifa za siri za Kampuni ya TTCL na wateja wake haziko salama.

Baada ya utafiti wa kina na majaribio ya kitaalamu, tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote.

Pamoja na taarifa hizi,    Wataalamu wetu wanaendelea kuwa macho kwa muda wote, ili kuhakikisha kuwa, wanafanyia kazi kila taarifa ama tishio la kiusalama linaloweza kujitokeza.
 TTCL inaendelea kuwaomba Umma na Wateja wetu wote kuendelea na majukumu yao kama kawaida bila wasiwasi wowote. TCCL inawaleta Karibu.

Comments

Popular Posts