UBALOZI WA MAREKANI WAIPONGEZA TTCL KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO WAKATI WA UJIO NA UWEPO WA RAIS BARACK OBAMA HAPA NCHINI.
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa
Marekani kwa huduma bora iliyotoa wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa
nchini.
Akitoa shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora
na za uhakika kutoka TTCL wakati wote wa
ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza kuwa
huduma walizozipata zimethibitishwa na
taarifa kutoka ofisi inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi
walizopita Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya
kiwango cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya
Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Akipokea salam hizo
za shukrani kutoka kwa ujumbe huo wa Marekani, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt.
Kamugisha Kazaura amesema, TTCL ilifanya
kazi yake kwa uhakika na ina uwezo wa kuhimili mahitaji ya watanzania na
Kimataifa pia.
Ameongeza kuwa
TTCL inaendelea na juhudi za kujikita zaidi katika huduma ya data/ intanet na
kuendelea kuboresha gharama ili kila mtanzania apate fursa ya kunufaika na
mawasiliano ya simu pamoja na data.
Katika Shukurani zake Bw. Jeff Shrader alioa pia
zawadi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura na kwa baadhi ya wawakilishi kutoa fani
mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL kama
ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment