TTCL YASHIRIKI KATIKA BONANZA LILILOANDALIWA NA SHIMMUTA, YANG'ARA KATIKA MICHEZO MBALIMBALI.

Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha TTCL kikiwa tayari kwa mechi kati yake na IFM ambapo walitoka sare bila ya kufungana. 
Mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya kukimbia ukiwa ndani ya gunia Bi. Alice Ngubwene akimalizia n'gwe wakati wa mashindano hayo.
wafanyakazi wa TTCL wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Dkt. Kamugisha Kazaura wakipongezana baada ya kushinda michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa bao, kula "Apple" likiwa linaning'inia, kukimbia kwa kutumia magunia n.k. TTCL pia ilishiriki michezo kama kukimbia huku ukitunga uzi kwenye sindano, kufukuza kuku n.k.
Timu ya wanawake katika mchezo wa kuvutana kwa kamba wakichuana na timu ya TBS na kufanikiwa kuwagaragaza katika mchezo huo raundi ya kwanza, TTCL ilishinda nafasi ya pili baada ya timu ya MUHAS kushinda nafasi ya kwanza Katika raundi ya pili ya mchezo huo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt Kamugisha Kazaura ( wa tano kutoka kushoto) akifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam, anayefuata ( mwenye "track suit" nyeusi) ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu Edward Emmanuel. 


Comments

Popular Posts