UPATIKANAJI WA VOCHA ZA TTCL KATIKA HUDUMA ZA BENKI.



TTCL imerahisisha upatikanaji wa vocha za TTCL kupitia huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi. Mteja wa TTCL anaweza kununua vocha moja kwa moja kupitia kwenye akaunti yake ya benki kwa  kutumia simu za mkononi.

Jumla ya benki 13 kutoa huduma ya upatikanaji wa vocha za TTCL kwa urahisi zaidi. Benki hizo ni CRDB, Exim Bank, Dar es salaam Community Bank, Standard Chartered Bank, Akiba Commercial Bank, Tanzania Postal Bank, Mkombozi Bank, KCB Bank, Bank of Africa, Amana Bank, Umoja Switch, Barclays Bank na Peoples Bank of Zanzibar.

Hivyo basi, mteja mwenye akaunti ya benki, na ambaye anatumia simu ya mkononi ya mtandao wa Tigo,Vodacom, Airtel au Zantel sasa anaweza kununua vocha ya TTCL wakati wowote na mahali popote kwa njia ya simu ya mkononi. 

Jinsi ya kupata vocha.
Mteja wa TTCL ili kupata huduma hii, anapaswa kuwa amejisajili kwenye huduma ya benki kwa njia ya simu (Mobile Banking) ya benki yake. Kisha, mteja anapaswa kutumia simu yake ya mkononi kwa kubofya namba kwa mujibu wa benki aliyopo. kwa mfano; CRDB unabofya *150*03# kisha fuata maelekezo.

Utaratibu wa kubofya kwa mabenki tajwa ni kama ufuatavyo;-


Exim Bank
*150*11#
Dar Es Salaam Community Bank
*150*51#
Standard Chartered Bank
*150*65#
Akiba Commercial Bank
*150*10#
Tanzania Postal Bank
*150*21#
Mkombozi Bank
*150*06#
KCB Bank
*150*22#
Bank of Africa
*150*13#
Amana Bank
*150*12#
Umoja Switch
*150*17#
Barclays Bank
*150*20#
Peoples Bank of Zanzibar
*150*40#
CRDB
*150*03#


Kwa wateja wa  benki 12  wanaweza kununua vocha kwa viwango ambavyo vimeainishwa kwa vocha za TTCL kama ilivyoonyeshwa hapa chini.



500/=
1000/=
2,000/=
5,000/=
10,000/=
30,000/=
60,000/=
100,000/=
200,000/=
360,000/=
450,000/=
1,000,000/=

Kwa wenye akaunti ya CRDB wanaweza kununua vocha TTCL kwa  kiwango chochote bila kufuata viwango hivyo hapo juu.  

Kutumia huduma hii kupitia CRDB fuata maelekezo yafuatayo:

o   Bofya *150*03#
o   Chagua namba 5
o   Chagua namba 5
 (namba 5 inasimama badala ya TTCL. Hivyo basi, atakayechagua namba 5 atakuwa amechagua TTCL)
o   Endelea na maelekezo mengine


Aidha, Maxmalipo na Selcom wireless Point pia bado wanaendelea kuuza vocha za TTCL.

Comments

Popular Posts