UFUNGUZI WA MKUTANO WA CONNECT TO CONNECT SUMMIT UNAOFANYIKA HOTELI YA BAHARI BEACH LEDGER PLAZA, DAR ES SALAAM TAREHE 30/09/2014 HADI TAREHE 01/10/2014


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, akifungua mkutano wa masuala ya TEHAMA, “Connect-to-Connect Summit” kwa niaba ya Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Wizara hiyo. Madhumuni ya mkutano huo ni kuwakutanisha wataalamu,  watunga sera, wadhibiti wa huduma za mawasiliano, makampuni ya simu, watoa huduma za mawasiliano na watumiaji wa huduma hizo kwa ajili ya kujadiliana namna ya kuongeza matumizi ya TEHAMA mijini na vijijini,ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano,  kukuza na kuboresha mazingira ya uwekezaji,matumizi ya teknolojia rahisi nautengenezaji na usambazaji wa vifaa vya huduma za mawasiliano.  Mkutano huo umehusisha washiriki kutoka nchi 53 za Bara la Afrika, Ulaya, Asia na Amerika. 



Prof. Patrick Makungu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akizungumza na Dkt. Ally Simba, Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo na mwakilishi wa HUAWEI.


Dkt. Kazaura, Afisa Mktendaji Mkuu wa TTCL akizungumza na mshiriki wa mkutano huo.


Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo. Mkutano huo umeandaliwa na TTCL kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.



Prof. Patrick Makungu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akizungumza na Mhe. Rebecca Okaci, Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta, Sudan ya Kusini.




Prof. John Nkoma, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akiwasilisha mada kuhusu ukuaji na usimamizi wa Sekta ya TEHAMA nchini Tanzania kwenye mkutano huo.


Mhe. Rebecca Okaci, Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan ya Kusini na Mhe. Win J. B. Mlambo, Naibu Waziri wa TEHAMA na Huduma za Posta wa Zimbabwe wakifuatilia majadiliano ya mkutano huo.


Washiriki wakifuatilia mkutano huo.


Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.





Comments

Popular Posts